Usimamizi wa Kisasa wa Harusi, Bajeti & Michango kwa Dijitali
Tengeneza kadi za kielektroniki za QR Code, simamia michango na ahadi za wageni, fuatilia bajeti na matumizi ukumbini kwa urahisi zaidi na bila msongo wa mawazo.
Tengeneza kadi za kielektroniki za QR Code, simamia michango na ahadi za wageni, fuatilia bajeti na matumizi ukumbini kwa urahisi zaidi na bila msongo wa mawazo.
Ingia au Jisajili Kusimamia Sherehe Yako
Sogeza ukurasa kwenda chini uone kabaasha linavyojifungua, kadi inavyotoka, keki inavyoshuka chini, na maputo yanavyoenda juu!
Serena Hotel, Dar es Salaam
Jumamosi, 28 Desemba 2026
Ondokana na madaftari ya zamani. Tumia teknolojia inayorahisisha kazi za kamati na wageni wote.
Tengeneza kadi zenye QR/Barcode ya kipekee kwa kila mgeni. Scan kadi mlangoni ukumbini kwa sekunde 1 tu!
Fuatilia kwa usahihi ahadi na malipo ya kila mchangiaji (Single, Double, Familia). Baki na ripoti halisi mkononi.
Panga bajeti ya ukumbi, chakula, vinywaji, na rekodi matumizi madogo madogo. Mfumo unakuonyesha cash iliyobaki mkononi.
Tuma ujumbe wa kukumbusha michango iliyobaki na SMS za shukrani moja kwa moja kwa simu za wageni wako.
Ongeza Wenyeviti, Makatibu, na Wahazini wenye ruhusa mbalimbali za kusimamia na kuingiza data kwa usalama.
Taarifa zako ziko salama 24/7 kwenye wingu (Cloud). Unaweza kuzipata ukiwa mahali popote kupitia simu au kompyuta.
Hesabu makadirio ya bajeti na kiasi utakachokusanya kulingana na idadi ya wageni wako.
Hutaji ujuzi wowote wa kiufundi. Mfumo wetu umeundwa kwa ajili ya kila mtu.
Jisajili kwa namba ya simu au email. Weka jina la sherehe (mfano: Harusi ya Kelvin & Grace) na tarehe.
Weka orodha ya wamchangiaji, kiasi walichowahidi au kulipa, na panga bajeti ya mahitaji ya sherehe.
Tuma kadi za QR kwa wageni kupitia WhatsApp. Siku ya sherehe scan kadi zao mlangoni kwa kutumia simu!
MualikoApp imesaidia mamia ya harusi na sherehe kufanikiwa bila msongo wa mawazo.
"MualikoApp ilitusadia sana kwenye harusi yetu Dar es Salaam. Tulikuwa na wageni 350 na kadi zote za QR ziliscanwa mlangoni bila foleni kabisa. Kamati ilifurahi mno!"
"Kama Mwenyekiti wa Kamati, kufuatilia michango na kutuma SMS za kumbukumbu ilikuwa kazi rahisi mno. Kila mtu kwenye kamati aliona takwimu zikiwa wazi."
"Tofauti na mifumo mingine, MualikoApp ni rahisi sana kuelewa hata kwa mtu asiye na ujuzi wa kompyuta. Ripoti za matumizi ya cash zilisaidia kutopoteza hela."
Unahitaji msaada zaidi? Pata majibu ya maswali ya kawaida hapa.
Kujisajili na kuanza kutumia MualikoApp ni BURE kabisa! Unaweza kuongeza sherehe yako, kuweka bajeti, na kusimamia michango bila malipo yoyote ya awali.
Naam! MualikoApp ni Mfumo wa Kisasa (Progressive Web App) unaofanya kazi vizuri kwenye simu yoyote ya Android, iPhone, Tablet au Kompyuta bila hitaji la kudownload app kubwa.
Mfumo unazalisha link maalum ya kadi au picha ya QR Code kwa kila mgeni aliyekamilisha mchango wake. Unaweza kuituma moja kwa moja kupitia WhatsApp au SMS kwa kubonyeza kitufe kimoja tu!
Ndio kabisa! Unaweza kuongeza Wenyeviti, Makatibu, au Wahazini kwenye sherehe yako na ukawapa ruhusa maalum za kuingiza michango na kusimamia matumizi.